Download Nena Rohoni #8211; Lilian Kirui #038; Noah Ochanda

Artist(s) Name: ,

Track Title: Nena Rohoni #038; Noah Ochanda

Category: Lyrics

Output Format: audio mp3

Published: 2023

Nena Rohoni – Lilian Kirui & Noah Ochanda Lyrics

Nyimbo Za Kikristo No. 15: Nena Mungu
1. Nena rohoni yesu, Nena kwa upole
Sema kwangu kwa pendo, “Huachwi upweke.”
‘Fungua moyo wangu, Nisikie mara;
Jaza roho na sifa, Sifa zako Bwana.

Kila siku unene, Vile kwa upole,
Nong’oneza kwa pole wa pendo:
“Daima utashinda, Uhuru niwako.”
Nisikie maneno: “Huachwi upweke.”

2. Nena kwa wana wako, Waonyeshe njia,
Wajaze kwa furaha, Fundisha kuomba;
Wajifunze kutoa Maisha kamili,
Wahimize ufalme, Tumwone Mwokozi.

3. Nena kama zamani, Ulipoitoa
Sheria takatifu: Niiweke pia;
Nipate kutukuza Wewe Mungu wangu,
Mpanzi yako tena, Daima ’kusifu.